Afisa
mtendaji mkuu wa kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) Dkt. Kamugisha Kazaura
ametoa mada kuhusu mkakati wa TTCL kusambaza mawasiliano ya kasi katika
majengo nchini wakati wa mkutano wa bodi ya Usajili wa Makandarasi (
Contractors Registration Board (CRB) ambapo pia bodi hiyo ilikuwa
ikiadhimisha miaka kumi na tano tangu kuanzishwa kwake.
Katika
mkutano huo uliohudhuriwa na makandarasi takribani 800 kutoka sehemu
mbalimbali hapa nchini, Dkt. Kazaura aliwaeleza nia ya TTCL kusambaza
mawasiliano ya kazi katika majengo mbalimbali hapa nchini na kuomba
ushirikiano wa hali ya juu kutoka kwa makandarasi kujenga majengo ambayo
yatakuwa yamewezeshwa tayari kuunganishwa na huduma za mawasiliano ya
kasi " Broadband Ready Buildings".
Afisa
Mtendaji mkuu wa TTCL Dkt. Kamugisha Kazaura akiwasilisha mada kwenye
mkutano huo, kushoto ni Eng. Samuel D. Shila kutoka kampuni ya Service
Consult Ltd na kulia ni Bw. Mringi Kitaly kutoka Msafiri Infrastructure
and Mining Solution.
baadhi ya washiriki wakifuatilia mada hiyo kwa umakini.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa TTCL Dkt. Kamugisha Kazaura akifafanua jambo kuhusu
mkongo wa taifa wa mawasiliano kwa waandishi wa habari na wateja
waliotembelea katika banda la TTCL.
Dkt Kazaura (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa bi. Josephine Mwakapugi kuhusu huduma zitolewazo na TTCL.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni