Jumatatu, 27 Mei 2013
Feza Kessy na Amil Nando waiwakilisha Tanzania kwenye Shindano la Big Brother-The Chase 2013
Mwakilishi kutoka Tanzania Amil Nando akihojiwa na Mtangazaji wa kipindi hicho Ik wakati wa uzinduzi wa show hiyo.Kushoto patna wa Nando Mshiriki kutoka Namibia Cleo.
Mwakilishi wa Tanzania Feza Kessy akiwasalimu mashabiki wake kwa kuwapungia bendera ya Tanzania. Kulia ni mtangazaji wa Shindano la Big Brother The Chase 2013 Ik.
Mtangazaji IK akifanya mahojiano na Patna wa Mwakilishi wa Tanzania Mshiriki kutoka Ghana Elikem wakati wa uzinduzi wa Shindano la Big Brother The Chase lililozinduliwa rasmi leo jijini Johannesburg Afrika Kusini ambapo washiriki watakaa ndani ya jumba hilo kwa siku 90 na mshindi kujinyakulia kitita cha Usd 300,000. Kulia ni Feza Kessy mshiriki kutoka Tanzania.
Mtangazaji IK akimtambulisha rasmi mshiriki kutoka Tanzania Feza Kessy kwa Patna wake Mshiriki kutoka Ghana Elikem wakati wa uzinduzi wa shindano hilo leo jijini Johannesburg.
Kundi la Mafikizolo la nchini Afrika Kusini likitoa burudani wakati wa uzinduzi wa show ya Big Brother-The Chase iliyorushwa Live na Channel za DStv 197 na 198 jijini Johannesburg usiku huu. Shindano la Big Brother-The Chase limedhaminiwa na Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel.
Baadhi ya wageni waalikwa wakiwemo waandishi wa habari kutoka nchin mbalimbali za Afrika kushuhudia Live uzinduzi huo.
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka nchi mbalimbali za Afrika waliopata mwaliko wa kuhudhuria uzinduzi wa shindano hilo Live kutoka Kampuni ya Multichoice Africa. Wa pili kulia ni Operations Manager wa Mo Blog Zainul Mzige aliyeiwakilisha Tanzania.
Kutoka kushoto ni Mwandishi wa habari kutoka Afrika Kusini Munya, Buhle na Thato kutoka Ofisi za Multichoice Afrika Kusini wakishow love back stage wakati wa uzinduzi wa shindano la Big Brother The Chase.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni