Uamuzi huo unatokana na sababu za kiufundi unaosimamia uendeshaji wa huduma hiyo jijini.
Kwa utaratibu huduma hii huendeshwa kwa kutumia vichwa vya treni vitatu ambapo viwili uhudumia moja kwa moja na cha tatu huwa cha akiba . Kuanzia siku ya Jumamosi ambapo huduma haikuwepo, kichwa cha tatu kiligundlika kuhitaji matengenezo makubwa na kupelekwa katika karakana yetu ya Morogoro.
Kutokana na utaratibu tulioainisha hapo awali kukosekana kichwa cha dharura ’standby’ kunalazimisha tusitishe huduma kwa muda. Hata hivyo Wahandisi na Mafundi wa Karakana yetu Kuu Morogoro wanatarajia kukamilisha kazi hiyo kabla ya siku ya Jumatano na hivyo kutoa fursa huduma hiyo kuanza tena siku ya Jumatano Julai 10, 2013.
Uongozi wa TRL unawaomba radhi wakazi wa Jiji na kuwataka kuwa na uvumilivu wakati huu wa ukarabati kichwa cha treni unaoendelea na kwamba muda sio mrefu Wanareli wa TRL watafanya kila linalowezekana kuirejesha huduma hii walioizoeya.
Tamati
Imetolewa na Afisi ya Uhusiano ya TRL kwa Niaba ya
Mkurugenzi Mtendaji ,
Mhandisi Kipallo Aman Kisamfu
Dar es Salaam,
Julai 08, 2013.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni