Jumatatu, 8 Julai 2013
DKT. SHEIN AFANYA UZINDUZI WA GATI MPYA YA ABIRIA MALINDI,ZANZIBAR
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akifungua pazia kama ishara ya uzinduzi wa Bandari mpya ya Abiria katika bandari ya Malindi Zanzibar leo.mchana (kushoto) Sheikh Said Salum Bakhresa.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,alitembelea sehemu mbali mbali katika ikiwemo IMMIGRATION DEPARTURES pamoja na Viongozi aliofuatana nao baada ya kugungua Bandari ya Abiria katika Bandari ya Malindi Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akipata maelezo kutoka kwa Injinia Mkuu wa Shirika la Bandari Mbarouk Hamad,(katikati) wakati alipotembelea sehumu ya Kuegeshea Meli ya Mizigo katika sherehe za ufunguzi wa Bandari mpya ya Abiria katika bandari ya Malindi Zanzibar leo.mchana.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akimkabidhi zawadi mfadhili wa Kampuni ya ujenzi wa Bandari mpya ya Abiria,Sheikh Said Salum Bakhresa,katika sherehe za ufunguzi wa Bandari mpya ya Abiria katika bandari ya Malindi Zanzibar leo mchana.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,alipokuwa akizungumza na wananchi na waalikwa katika sherehe za ufunguzi wa Bandari mpya ya Abiria katika bandari ya Malindi Zanzibar leo.mchana,(kushoto) Naibu Waziri wa Mawasiliano na Miundimbinu Issa Haji Ussi (Gavu) Harison Mwakiembe Waziri wa Miundombinu Bara,na Sheikh Said Salum Bakhresa (kulia).[Picha na Ramadhan Othman, Ikulu.]
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni