Wachezaji
wawili wa Ivory Coast wametimuliwa kwenye kikosi kinachojiandaa na
mchezo kuwania kufuzu michuano ya kombe la dunia mwaka 2014 dhidi ya
Tanzania unaotarajiwa kupigwa uwanja wa Taifa siku ya Jumapili.
Mchezaji
wa zamani wa Monaco Jean-Jacques Gosso Gosso, 30, ambaye kwa sasa
anakipiga kwenye ligi ya Uturuki akiichezea Mersin na kinda la miaka 20
Abdul Razack wa Manchester City, ambaye kwa sasa yupo kwa mkopo Charlton
Athletic, walipigana siku ya jumatano wakati timu yao ikiwa kwenye
maandalizi ya mwisho kabla ya kuja Tanzania usiku wa leo.
FA ya Cote D’Ivoire imesema kwamba adhabu nyingine zinaweza kufuatiwa kutegemea na kamati ya nidhamu itakavyoamua.
Wakati huo huo timu hiyo ya Ivory Coast imeshafika nchini na wamefikia kwenye hoteli ya Bahari Beach.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni