Mratibu
wa shindano la Redd's Miss Kinondoni 2013, Deniss Ssebo akiongea na
waandishi wa habari kuhusiana na shindano hilo, alisema kuwa mwaka huu
imeleta mapinduzi Makubwa katika sekta ya Afya, Elimu pamoja na Ajira.
Ambapo
mshindi wa kwanza atapata udhamini wa masomo (Scholarship) kwa muda wa
mika miwili katika kuendeleza masomo yake na kama amemaliza kusoma basi
atapa ajira kwenye hoteli ya kimataifa ya JB Belmonte kulingana na elimu
aliyonayo. Pia atapata shopping vocha kutoka Oriflame ya tshs. 300,000
pamoja na fedha taslimu tshs. 500,000.
Mshindi
wa pili; atapata udhamini wa masomo (Scholarship) ya mwaka mmoja,
fedha taslimu 300,000 na shopping vocha kutoka Oriflame ya tshs.
200,000.Mshindi wa tatu; atapata udhamini wa masomo (Scholarship) ya
mwaka mmoja, fedha taslimu 200,000 na shopping vocha kutoka Oriflame ya
tshs. 100,000.
Mshindi
wa 4 na tano; watapata uthamini wa masomo ya kompyuta ya miezi sita.
Mshindi wa nne atapata pia pesa taslimu laki mbili na nusu na wa 5 laki
moja na nusu.Washiriki wengine wote watapata kifuta jasho cha shilingi
laki mbili kwa kila mmoja.
Muonekano wa warembo wa Redd's Miss Kinondoni 2013
Mashindano
ya Redd's Miss Kinondoni 2013 yanatarajia kufanyika kwenye ukumbi wa
hoteli ya Golden Tulip siku ya Ijumaa 21 June 2013. Viingilio katika
onyesho hilo ni shs. 60,000 VIP, shs. 25,000 kwa tiketi za kawaida na
meza ya watu ukitazama zawadi.
Mashindano
ya Redd's Miss Kinondoni yanatarajiwa kufanyika June 21, huku walowa
yamedhaminiwa na Redd's Original, Chilly Willy Energy Drink, Oriflame
Natural Beauty Products, Times Fm, JB Belmonte Hotel, Michuzi Media
Group, Michuzijr Blog, Mtaa Kwa Mtaa Blog, Fullshangwe Blog, Mrokim
Blog, SufianMafoto Blog, Global Publisher, Mdimuz Blog, Lukaza Blog, MO
Blog, DjChoka Blog na Kajunason Blog.
Mmoja ya warembo wa Redd's Miss Kinondoni 2013 akiuliza swali kwa mwezeshaji.
Kila mrembo akijaribu kuweka kumbu kumbu kwa yale waliyokuwa wakifundishwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni