NYOTA
wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo na kocha wake Jose Mourinho
wamefungiwa mechi mbili mbili kila mmoja katika Kombe la Hispania kwa
matukio waliyofanya katika fainali ya Kombe la Mfalme wakifungwa 2-1 na
Atletico.
Kocha
Mourinho alipandishwa jukwaani kwa kubishana na marefa juu ya uamuzi,
pia mwalimu huyo mwenye umri wa miaka 50 anaweza kuepuka kuitumia adhabu
hiyo kutokana na tangazo la kuondoka kwake Real.
Mfalme wa mabao Real, Ronaldo alipewa kadi nyekundu mwishoni mwa mchezo huo kwa kumpiga tekenahodha wa Atletico, Gabi.
Jose Mourinho akiamriwa kupanda jukwaani na refa Clos Gomez kwenye fainali ya Kombe la Mfalme
Cristiano Ronaldo alitolewa kwa kadi nyekundu dakika za mwishoni kwa
kumpiga teke kiungo wa Atletico, Gabi
Mchezaji
huyo mwenye umri wa miaka 28, amefungiwa mechi moja kwa kufanya fujo na
moja kwa kupewa kadi mbili, ya kwanza akipewa mwanzoni mwa mechi.
La kusawazisha: Atletico wakishangilia bao la kwanza dhidi ya Real
Wote
watakuwapo kwenye mechi mbili za mwisho za Real La Liga msimu huu -
ugenini dhidi ya Real Sociedad Jumapili na nyumbani dhidi ya Osasuna
mwishoni mwa wiki itakayofuata- kwa sababu kifungo chao katika Vikombe
tu.
Nahodha wa Atletico, Gabi akiwa ameinua Kombe la Mfalme
Ronaldo
aliifungia Real bao la kuongoza dakika ya 55 Uwanja wa Bernabeu, lakini
Atletico ikasawazisha kupitia kwa Diego Costa kabla ya Joao Miranda
kufunga la ushindi dakika za nyongeza.
Kipigo
hicho kutoka kwa mahasimu wao wa Jiji, kinamaanisha Real imemaliza
msimu bila taji lolote, wakati Jumatatu ilithibitishwa Mourinho
anaondoka.
kaka nimekubali lazima nikutafute hata sikubali,pa 1 sana one love jigwa
JibuFuta