Rais Jakaya Kikwete akiongea na wachezaji wa timu ya mpira ya Taifa, Taifa Stars leo Ikulu jijini Dar es salaam alipokutana nao kuwapa hamasa waweze kupata ushindi katika mchezo wao dhidi ya Moroco utakaochezwa Juni 7, na michezo mingine ikiwa ni hatua ya kuiwezesha timu hiyo kukata tiketi ya kushiriki mashindano ya kombe la dunia mwaka 2014.
Rais Jakaya Kikwete akiwaaga wachezaji wa Timu ya Taifa Stars mara baada ya kukutana nao leo Ikulu Jijini Dar es salaam kuwahamasisha washinde mchezo dhidi ya timu ya Taifa ya Moroco utakaofanyika June 7 ikiwa ni sehemu ya Taifa Stars kutafuta ticketi ya kucheza mashindano ya Kombe la Dunia.
Meneja wa Timu ya Taifa Stars Bw. Mukebesi akiteta jambo na Kepteni wa Timu ya Taifa Stars Juma Kaseja Ikulu jijini Dar es salaam walipokutana na Rais Jakaya Kikwete.
Rais Jakaya Kikwete akiwa katika Picha ya Pamoja na wachezaji wa Timu ya Taifa , Taifa Stars, viongozi wa Wizara ya Habari, Vijana ,Utamaduni na Michezo na Viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Rais
Jakaya Kikwete akiwa katika Picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya
Taifa , Taifa Stars Ikulu jijini Dar es salaam. Picha na Aron Msigwa –
MAELEZO.
Na. Veronica Kazimoto –MAELEZO.
Rais
wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete leo
amekutana na timu ya Taifa (Taifa stars) kwa lengo la kuitia moyo katika
mechi ijayo kati yake na timu ya Moroco ikiwa ni harakati za Tanzania
kutafuta tiketi ya kucheza fainali za kombe la Dunia kwa mara ya kwanza
mwaka 2014.
Rais
Kikwete ameiambia timu hiyo kuwa ina uwezo mkubwa wa kusonga mbele
kutokana na uwezo mkubwa waliouonesha katika mchezo wao dhidi ya Gambia
ambapo walifanikiwa kupata ushindi wa bao 2-0.
“Maadamu
mara ya kwanza mliwashinda Gambia, hakikisheni pia mnapata ushindi
dhidi ya Moroco, mkishinda tunafurahi sana na mkishindwa tunanyong’onyea
sana,” amesema Rais Kikwete.
Aidha
amempongeza kocha wa timu hiyo Kim Poulsen pamoja na Kamati ya Taifa ya
ushindi ya Taifa stars kwa kuisaidia timu hiyo kiasi cha shilingi
milioni 30 ikiwa ni mkakati wa kuiongezea nguvu kwa hatua iliyofikia na
kuwataka wachezaji kujituma ili kuwafurahisha watanzania ambao hivi sasa
wanaipenda timu yao ya Taifa.
Nae
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Fenera Mukangara amesema
Serikali itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa michezo nchini
ili kuondoa changamoto zinazoikabili timu hiyo.
Kwa
upande wake Kocha Poulsen, amemshukuru Rais Kikwete kwa kuwakaribisha na
kuwatia moyo ambapo ameahidi kuifundisha vizuri timu hiyo ili
kuhakikisha kuwa wanapata ushindi.
Akizungumza
kwa niaba ya wachezaji wenzake kaptaini wa timu hiyo Juma Kaseja
amemshukuru Rais Kikwete na kuahidi kujituma kwenye mazoezi na hatimaye
kuibuka washindi kwenye mechi zijazo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni