Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akimkaribisha Mkuu wa jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali Said Mwema,
ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, wakati alipofika kwa
mazungumzo leo Mei 27, 2013. Picha na OMR.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akizungumza na Mkuu wa jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali Said Mwema,
ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, wakati alipofika kwa
mazungumzo leo Mei 27, 2013
======== ======= ====== =======
MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA MKUU WA JESHI LA POLISI NA KUMPA POLE KUFUATIA VIFO VYA ASKARI WALIOFARIKI MTWARA.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal
amekutana na Mkuu wa jeshi la Polisi Inspekta Jenerali Said Mwema
ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam leo Jumatatu Mei 27, 2013.
Katika
mkutano huo, Mheshimiwa Makamu wa Rais ametumia nafasi hiyo kumpa pole
Mkuu wa Polisi kufuatia ajali ya gari la iliyosababisha vifo vya askari
wanne wa Jeshi hilo, waliokuwa njiani kutoka Nachingwea kuelekea Mkoani
Mtwara kwa kazi maalum ya kudhibiti vurugu zilizojitokeza Mkoani humo
juma lililopita.
Mheshimiwa
Makamu wa Rais alisema, askari hao watazidi kukumbukwa kwa kuwa
walikuwa mstari wa mbele kuhakikisha majukumu yao kwa Taifa hili
yanafanikiwa. Mheshimiwa Makamu wa Rais alisema pia kuwa, serikali
inathamini sana mchango wa Jeshi la Polisi sambamba na majeshi mengine
kutokana na kufanya kazi kwa kujitolea na kwa kutambua kuwa ulinzi na
usalama wa Taifa ni jambo muhimu kwa maendeleo ya nchi.
Mheshimiwa
Makamu wa Rais alimueleza Mkuu wa Polisi kuwa, kazi inayofanywa na
jeshi lake ni kubwa na kwamba Watanzania wanaithamini sana. Pia
aliongeza kuwa katika nchi zote wananchi wanaojitolea kufanya kazi
katika vyombo vya usalama, ni miongoni mwa wazalendo wakubwa wanaopaswa
kuenziwa kwa kuwa wamekubali kuweka maisha yao kwa ajili ya nchi na watu
wake.
Katika
mkutano huo, Makamu wa Rais alitumia nafasi hiyo kupata taarifa kuhusu
hali ya usalama mkoani Mtwara na pia kubadilishana mawazo kuhusu
kuhakikisha maeneo ya nchi yetu kubakia salama wakati wote.
Imetolewa na Boniphace Makene
Mwandishi wa Habari wa Makamu wa Rais
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni