Mwanafunzi
wa Chuo Cha Ualimu Kasulu, mkoani kigoma Valerian Nickodemus Kamugisha
akinyannyua kwa Furaha sehemu ya fedha Sh 100 Milioni alizoshinda katika
droo kuu ya Promosheni ya Vodacom Mehala iliyomalizika hivi karibuni.
Kamugisha amekabidhiwa fedha zake hizo leo jijini Dar es salaam na
kuamua kuzifungulia akaunti katika benki ya NMB. Wa kwanza kulia ni Mkuu
wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa NMB Bw.Abdulmajid Nsekela na Mkuu wa
Chapa Vodacom na Mawasiliano Kelvin Twissa.
Mkuu
wa Chapa Vodacom na Mawasiliano Kelvin Twissa akimtambulisha kwa
waandishi wa habari(hawapo pichani) mshindi wa Promosheni kuu ya Mahela
iliyomalizika hivi karibuni Valerian Nickodemus Kamugisha (kushoto)
wakati wa hafla ya kumkabidhi kitita chake cha zawadi ya sh. 100 Milioni
iliyofanyika makao makuu ya NMB. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Wateja
Binafsi wa NMB Bw.Abdulmajid Nsekela.
Valerian
Nickodemus Kamugisha (katikati) akipokea kitita cha sh. 100 Milioni
kutoka kwa Mkuu wa Chapa Vodacom na Mawasiliano Kelvin Twissa
alizoshinda katika droo kuu ya Promosheni ya Vodacom MAHELA. Hafla ya
makabidhiano imefanyika makao makuu ya benki ya NMB ambako mshindi huyo
amechagua kufungua akaunti kuhifadhi fedha hizo. Kushoto ni Mkuu wa
Kitengo cha Wateja Binafsi wa NMB Bw.Abdulmajid Nsekela.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni