Kufuatia
wito wa rais Jakaya Kikwete kwa marais wa mataifa ya maziwa Makuu
marais Paul Kagame, wa Rwanda, Joseph Kabila wa jamhuri ya Kidemokrasia
ya Kongo na Yoweri Museveni wa Uganda, kuzungumza na makundi ya waasi
yanayopambana na nchi zao.
Baadhi
ya Wanyarwanda wanaoishi Marekani walipinga ushauri huo na kudai
watamwandikia Rais Obama na kumtaka rais Kikwete abadili usemi huo na
kuwataka radhi.
Lakini
kwa upande mwingine baadhi ya wabunge wa Kongo Kwenye taarifa yao ya
pamoja iliyosomwa na mbunge Benjamin Mukulungu , wabunge hao wa Kivu
Kusini na Kaskazini wameomba kuwe na mtazamo wa jumla wa viongozi wa
kanda ya maziwa makuu na umoja wa mataifa ili kumaliza vita nchini
Congo.
Wabunge
wa Kivu wamepongeza msimamo wa rais wa Tanzania Jakaya Kikwete wa
kutaka kuwe na mazungumzo kati ya serikali za Congo Rwanda na Uganda na
makundi ya waasi wanayopingana nayo.
Wabunge
wa Kivu wametaka pendekezo la rais Kikwete ni lazima lipewe kipaumbe
bnena jumuiya ya kimataifa ili kuwe na amani kwenye eneo hilo.
Mbunge
wa upinzani Emerio Kunji kutoka jimbo la Kasai amesema amepanga kutoa
hoja rasmi bungeni ili kuweko na azimio la bunge kuhusu msimamo ambao
serikali ya Congo inatakiwa kuchukua kwa ajili ya kutatua mzozo wa Kivu.
Akisema
“rais wa Tanzania alichukua msimamo wa kijasiri wa kuonyesha kwamba
mzozo wa maziwa makuu hauwezi kutambuliwa kwa njia ya kinafiki bali
kupitia mtizamo ulio thabiti bunge letu ni lazima litoe shinikizo kwa
serikali ili kuweko na mtizamo mpya wa ufumbuzi wa mzozo huo”.
Kwa
muda wa siku tano sasa pendekeo hilo la rais Kikwete limeendelea
kuzusha maoni mengi kwenye vyombo vya habari ngazi ya kisiasa, na kwa
watu wa kawaida huko mjini Kinshasa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni